Okebiz Video SearchTitle:Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 1
Duration:41:30
Viewed:70,899
Published:27-02-2021
Source:Youtube

#SalamaNa#SendTip​ Through MPESA #0762797291
Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Joseph Haule ni mmoja ya binadamu ambao nawapenda sana kwenye dunia hii na huwezi kuamini hata yeye anajiskia hivyo juu yangu, nikiwa naye vibe na story zetu huwa zinabamba sana. Kuanzia story za maisha, muziki, historia na hata kuwacheka watu wakati mwengine, ndo zetu.
Nakumbuka baada ya kumsaka asubuhi moja hivi na yeye kutodaka simu (ambayo baadae aliniambia alimpigia Sallam simu akidhani yeye ndo aliyempigia badala ya Salama), hayo maelezo niliyapata baada ya yeye kukutana na tweet ya kulalamika kwangu juu ya yeye kutorudisha simu yangu.

Tumetoka mbali kiasi chetu, mkubwa kwangu kwa miaka 7 na heshima yangu kwake si ya kupima kwa kisoda. Unaweza ukawa unajiuliza sasa mbona hatukuoni naye na mambo kama hayo (hiyo mambo kama hayo nimeongea kama yeye) well... Urafiki wetu si ule wa kugandana kama kifungo na shati, au kichwa na nywele au kucha na kidole ndugu yangu, urafiki wetu ni ule wa kuendeleza pale tulipoishia na kuangalia na kwa mbali juu ya kitu mwenzio anafanya huku tukitakiana Kheri.

Nakumbuka vizuri mara yangu ya kwanza kukutana na Profesa, enzi za Times FM kule mjini, kipindi hiko mimi ndo nimepata ajira yangu ya kwanza na yeye ndo alikua Msanii wa mooto sana, hard blasters wako na moto wa tipa, na nani ndo kiongozi wa nyika? Nigga Jay. Urafiki wetu ulianzia hapo, na mpaka leo tunamshkuru Mungu.

Ukuaji wake hasa ndo nia na madhumuni ya mimi na wenzangu kuona Prof atatufaa sana kumalizia episode yetu ya 55 na ngwe ya kwanza ya kazi yetu hii. Zaidi kama tujuavyo, hakuna msanii hata mmoja ambaye hajawahi kuvutiwa na hustle zake za kuanzia juzi mpaka leo hapa tulipo. Na hiyo inajumuisha kipaji na UANDISHI ulosimamia kucha. Jay tunakuzimia indeed!

So wapi haya yoooote yalianzia? Mpaka sasa Mbunge nje ya Bunge? Well... Hata mbuyu ulianza kama mchicha, humu Prof anazungumza na sisi juu ya masuala ya familia na safari alizopitia, mikoa aliyowahi kuishi, mahusiano kati ya Marehemu Baba yake na Mama yake, wadogo zake, Kaka na Dada zake, elimu yake, experience yake mjengoni, nini maana ya baadhi ya vitu na mambo aliyowahi kuyapitia. Pia tuliongelea kupatikana kwa binti yake pekee Lisa, jinsi alivyokutana na mke wake, kipaji chake, kwanini Mikumi na kwa mbaaali uchaguzi mkuu uliopita.

Profesa ni mwana flani ivi ambaye toka zamani ramani ya mambo yake yako mfuko wa nyuma, kupotea au kupoteza malengo si jambo rahisi kwake, labda kuchelewa tu kwa hayo aloyapanga. Na hivi sasa kwa miaka mitano hii ambayo yuko nje ya bunge, pengine ndo wakati wetu wa kufaidi kipaji chake na kuokota mawili matatu kwa wale wote tunao muangalia na kupenda nyenendo zake.
Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.

Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1H...

Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

SHARE TO YOUR FRIENDS


Download Server 1


DOWNLOAD MP4

Download Server 2


DOWNLOAD MP4

Alternative Download :SPONSORED
Loading...
RELATED VIDEOS
Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 2 Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 2
27:13 | 32,134
Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 1 Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 1
29:51 | 104,823
Salama Na CHARLES HILLARY Ep 38 | MZEE WA BUSARA Part 1 Salama Na CHARLES HILLARY Ep 38 | MZEE WA BUSAR...
33:12 | 73,618
Salama Na JOTI Ep 47 | SIMPLY SPECIAL PART 1 Salama Na JOTI Ep 47 | SIMPLY SPECIAL PART 1
35:15 | 344,410
Salama Na Darassa Ep 16 | KAWIA UFIKE Part 1 Salama Na Darassa Ep 16 | KAWIA UFIKE Part 1
31:12 | 71,387
Salama Na JK Ep 48| MSOGA UNO PART 1 Salama Na JK Ep 48| MSOGA UNO PART 1
28:27 | 434,633
Salama Na Shangazi Ep 28 | FIRST BORN Part 1 Salama Na Shangazi Ep 28 | FIRST BORN Part 1
41:43 | 101,311
Eric Omondi  performance in Tanzania - Cheka Tu Mlimani City Eric Omondi performance in Tanzania - Cheka Tu...
48:00 | 427,211


coinpayu