Okebiz Video SearchTitle:RAIS DKT. MAGUFULI AWASIMAMISHA TBA KUJENGA NYUMBA ZA MAGEREZA UKONGA
Duration:03:00
Viewed:45,065
Published:16-03-2019
Source:Youtube

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Machi, 2019 amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza wa gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuagiza mradi huo ukabidhiwe kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya kubaini kuwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeshindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati, licha ya Serikali kutoa shilingi Bilioni 10 za ujenzi. Ametaka wataalamu wa TBA waliokuwa wakisimamia mradi huo pamoja na Askari Magereza waondoke na kuwapisha JWTZ. “Kwa hiyo hapa nisimuone mtu wa TBA, nisimuone mtu wa Magereza kuja kusimamia, muwaache Jeshi la Wananchi wafanye kazi zao, siku watakapokuja kunikabidhi na mimi nitawakabidhi Magereza, kwa hiyo watu wa TBA kuanzia leo nimewafukuza hapa” amesema Mhe. Rais Magufuli. Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika mradio huo ambao ulianza zaidi ya miaka 2 iliyopita kwa kushirikisha Jeshi la Magereza ambalo lilikuwa linaisadia TBA katika kazi za ujenzi, na ametaka TBA na Jeshi la Magereza wabadilike katika utekelezaji wa majukumu yao. “Nataka kila mlipo watu wa Magereza mfanye kazi, msimamie watu, kama ni ng’ombe muwafuge vizuri wazalishe vizuri hadi muuze mazao nje, kama ni kilimo mlime kwelikweli, muwe ni jeshi la kuzalisha, hii ni aibu kuleta jeshi jingine la wananchi kuja kuwajengea nyumba nyinyi, wakati nyumba mnakaa nyinyi, mlitakiwa muwe mmeshapanga mkakati kwamba TBA wamesuasua, ngoja tufyatue matofari, tuanze kujenga” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli. Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Charles Mbuge amesema JKT itakamilisha ujenzi huo ndani ya kipindi cha miezi 2 na nusu kuanzia kesho na kwamba kazi zitafanywa usiku na mchana. Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameitaka TBA kutoa maelezo ya namna fedha zilizotolewa na Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 10 zilivyotumika, na ameonya kuwa endapo itabainika matumizi ya fedha hizo hayaendani na kazi zilizofanyika hatua kali zitachukuliwa. Katika mradi huo, ujenzi wa majengo 12 ya makazi ya Askari Magereza yaliyopangwa kuwa na ghorofa 4 kila moja ulioanza Desemba 2016 umefikia asilimia 45 tu na unaendelea kwa kusuasua.

SHARE TO YOUR FRIENDS


Download Server 1


DOWNLOAD MP4

Download Server 2


DOWNLOAD MP4

Alternative Download :SPONSORED
Loading...
RELATED VIDEOS
Why Leaders Lie: The Truth About Lying in International Politics with John Mearsheimer Why Leaders Lie: The Truth About Lying in Inter...
25:47 | 5,996,087
How to talk about your job in English: 10 Key Verbs How to talk about your job in English: 10 Key V...
25:19 | 1,085,813
UZINDUZI WA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA, MSALATO - DODOMA UZINDUZI WA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA, M...
08:18 | 14,339
Rais alivyompandisha cheo Kanali Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali Rais alivyompandisha cheo Kanali Charles Mbuge ...
03:31 | 704,460
RAIS DKT MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAFUNGWA NA MAHABUSU KATIKA GEREZA LA BUTIMBA JIJINI MWANZA RAIS DKT MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAFUNGWA NA MAHA...
07:38 | 133,871
How was England formed? How was England formed?
10:17 | 9,571,817
Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Terminal One JNIA Mei 13,2016 Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Termin...
17:24 | 163,667
LIVE : RAIS DKT. JOHN P. MAGUFULI AKIWA NJIANI KURUDI DAR ES SALAAM LIVE : RAIS DKT. JOHN P. MAGUFULI AKIWA NJIANI ...
48:48 | 140,010

shopee ads

coinpayu