Okebiz Video SearchTitle:Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 1
Duration:35:35
Viewed:168,089
Published:13-02-2021
Source:Youtube

#SalamaNa#SendTip​ Through MPESA #0762797291
Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu ambaye nafahamiana naye sana, ambaye nilishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndio ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua.

Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, kipindi hiko kilikua cha masikitiko kwao na kwake pia. Nandy alikua na ukaribu mwingi na Ruge, alishawahi kumtembelea hospitali mara kadhaa na pia alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa karibu wa familia kipindi kile ambacho Ruge alikua hana tena mawasiliano naye moja kwa moja. Siku ambayo Ruge alitangulia mbele za haki, muda si mrefu kabla ya hilo kutokea Nandy ananiambia alizungumza na nesi wa zamu siku hiyo na pia alimuekea simu kwa ukaribu na alimsikia akiwa anapumua. Wapi alikua wakati anapata habari hii iko kwenye maongezi yetu haya, humu pia utaelewa connection ambayo sisi binadamu tunayo na watu ambao tunawapenda na wanao tupenda.

Najua siku hazigandi kama ambavyo Lady Jd alishawahi kuimba na ndio nikawaza, hivi ushawahi kuwaza Nandy amekua kiasi gani toka msiba wa Ruge utokee? Unakumbuka baadhi ya maneno yaliosemwa juu ya career yake baada ya msiba ule? Tunafahamu kwamba alipoteza rafiki, mentor, baba na kama tochi yake. Mimi huwaza haya sana, na hilo la yeye kujidhatiti na kukaza mwendo ndio ambalo lilifanya mimi binafsi niseme you know what, it’s time.

Nandy ni MPAMBANAJI, anaupenda muziki na kama mtu mwengine yeyote mwenye jitihada basi Mungu humfungulia milango ya Kheri. Kaniambia humu kwenye maongezi yetu kwamba safari yake ya kwanza kwenda nchini Nigeria kwenye mashindano ya kuimba alimuambia Mama yake wakati yumo ndani ya ndege, alipomaliza hotuba yake fupi alizima simu na wheels up, to Lagos ambako alihakikisha anapigana mpaka fainali na kumaliza nafasi ya tatu. Si kitu kidogo kwa binti ambaye aliamua kuweka shule pembeni ili atimize ndoto yake, ndoto ambayo hata Mama yake mzazi hakua na taarifa nayo.

Siku zinakwenda, maisha yanasonga na yeye ameendelea kukimbiza ndoto yake na mpaka tunaenda mitamboni, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wakubwa sana hapa nyumbani na barani Afrika na hata Ulaya na Marekani na ukitizama vizuri utajua kwamba huu ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yatatokea katika maisha yake. Mimi na yeye tulizungumzia mahusiano hayo pamoja na kukimbiza ndoto zetu. Tuliongelea Bill Nas na kiwanda cha muziki wa Bongo Flava. Tuliongelea muziki wake na collabo ambazo amewahi kufanya. Hapo hapo nilitaka kujua pia yeye ni mtu wa aina gani na ni vitu gani vinamsukuma kutaka atake zaidi na sehemu ambayo anajiona huko mbeleni In Shaa Allah.

Yangu matumaini kama kawaida ni kwamba utajifunza mawili matatu ambayo yatakusaidia kupambana na mitihani ya maisha kwasababu tu umejifunza kutokana na sehemu wenzetu hupitia kwenye maisha yao.
Tafadhali Enjoy.

Love,
Salama.

Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1H...

Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

SHARE TO YOUR FRIENDS


Download Server 1


DOWNLOAD MP4

Download Server 2


DOWNLOAD MP4

Alternative Download :SPONSORED
Loading...
RELATED VIDEOS
Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 2 Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 2
15:59 | 79,119
Salama Na VANNY BOY Ep 54 | NDAGHA PART 1 Salama Na VANNY BOY Ep 54 | NDAGHA PART 1
39:49 | 343,706
Salama Na Shikana Ep 17 | DYNAMITE Part 1 Salama Na Shikana Ep 17 | DYNAMITE Part 1
29:48 | 264,399
Salama Na RIYAMA Ep 32 | UTAKWENDA UTARUDI Part 1 Salama Na RIYAMA Ep 32 | UTAKWENDA UTARUDI Part 1
34:34 | 143,032
Salama Na Gigy Money Ep 12 | ZILE KHADITHI Part 1 Salama Na Gigy Money Ep 12 | ZILE KHADITHI Part 1
25:27 | 301,233
Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1 Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1
33:07 | 244,608
Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 1 Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 1
41:30 | 70,899
Salama Na JK Ep 48| MSOGA UNO PART 1 Salama Na JK Ep 48| MSOGA UNO PART 1
28:27 | 434,632


coinpayu