Okebiz Video SearchTitle:Salama Na Shikana Ep 17 | DYNAMITE Part 2
Duration:15:59
Viewed:136,635
Published:24-05-2020
Source:Youtube

#YAHStoneTown#SalamaNa#PodCast
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Mi na rafiki yangu huyu tumepishana zaidi ya miaka kumi na nne, wakati anazaliwa mimi nilikua nagombana na makondakta kupata nafasi kwenye chai maharagwe ya kutoka Buguruni kuelekea Posta. Ila kupishana kwetu kwa umri naamini ndo kunaufanya ushoga wetu uwe special zaidi, maana yeye akiwa ananikhadithia kinachokiki kwenye umri wake, nami nakua namuelezea challenges za unapozidi kukua na naamini hii inatufanya tuwe bora zaidi. Na ki ukweli mara nyingi yeye amekua shujaa wangu, maana kuna mengine mazito kwake yanakua mepesi tu na hunisaidia kuona mambo kwa picha tofauti. Kwa hilo namshukuru sana. Wakati mwengine wanasema umri sio kipimo cha busara, rafiki yangu huyu kupitia mengi, kwahiyo moyo wake wa ‘chuma’ unatusaidia wengi kwenye kuweza kupambana na dhurba mbali mbali.

Hapa sina haja hata ya kukuambia alipitia mitihani kiasi gani maana dunia nzima inajua, ila naweza tu kukuambia kwamba hakuna binti mwenye moyo wa utayari na ambae hana uwoga pale anapokua anasimamia lake kama Elizabeth Michael Kimemeta. Kwanza akiweka nia kwenye jambo lake lazima liwe... Atafunga, atakesha asali, ataweka akili na mawazo yake yote humo mpaka Mwenyezi Mungu amtimizie, nishashuhudia hilo sio mara moja wala mbili na naweza nikasema binafsi ameni inspire sana kwenye suala zima la funga na sala. Nani kamfundisha hayo? Kwa umri wake aliokua nao wakati matatizo mazito yalipomfika pengine usingedhani angekua binti wa dizaini hiyo. Miaka minne au mitano ambayo Alikutwa na yale matatizo ya kesi na mpaka akatumikia kifungo ni miaka ambayo ilimfaya akue sana. Ki imani na kiakili.

Kwenye kipindi hiki hakua bado tayari kuzungumzia usiku ule ulobadilisha maisha yake ila kaniahidi akiwa tayari basi atafiria kutushirikisha kwenye hayo maongezi ila inawezekana pia hiyo siku isifike, nna hisia hiyo ni kurasa ya kwenye kitabu ambayo amechagua kuiruka kwa sasa au pengine milele, na maamuzi hayo mimi na wenzangu tuliyaheshimu.

Sote tunakumbuka wakati anakua, kila kukicha yuko kwenye gazeti ila kwa sasa huyo si yule, amekua ki mwili, ki akili na hata ki sanaa pia. Mambo yake si ‘hadharani’ tena kama ilivyokua miaka ya nyuma. Sasa amekua influencer ambaye kampuni kubwa kadhaa zinamuamini yeye kuwatangazia biashara yao. Amekua Mama kwa mdogo wake Eric ambaye naye tumemuona akikua kwenye macho yetu. Mama kwa watoto wawili ambao amewakuta wakiwa wanaishi na mchumba wake nyumba moja.

Kwenye haya maongezi yetu tuligusia hilo la hao watoto, na watoto wengine, kazi, yeye kama binti ambae amekua akikutana na mawe mengi. Muonekano wake. Familia kwa upande wa Mama na Baba na mambo mengine kadhaa. Niko hapa kukutakia uangaliaji mwema wa kipindi hiki na yangu matumaini utavutiwa na jambo ambalo litakufanya ubadili maisha yako kwa uzuri zaidi. Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.

Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1H...

Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

SHARE TO YOUR FRIENDS


Download Server 1


DOWNLOAD MP4

Download Server 2


DOWNLOAD MP4

Alternative Download :SPONSORED
Loading...
RELATED VIDEOS
Salama Na Shikana Ep 17 | DYNAMITE Part 1 Salama Na Shikana Ep 17 | DYNAMITE Part 1
29:48 | 264,311
Salama Na KAJALA Ep 35 | JERAHA LA MOYO Part 1 Salama Na KAJALA Ep 35 | JERAHA LA MOYO Part 1
29:56 | 185,130
Salama Na Jokate Ep 3 | KAMISHNA Part 1 Salama Na Jokate Ep 3 | KAMISHNA Part 1
26:24 | 269,668
Salama Na RIYAMA Ep 32 | UTAKWENDA UTARUDI Part 1 Salama Na RIYAMA Ep 32 | UTAKWENDA UTARUDI Part 1
34:34 | 142,981
Salama Na VANNY BOY Ep 54 | NDAGHA PART 1 Salama Na VANNY BOY Ep 54 | NDAGHA PART 1
39:49 | 343,507
Salama Jabir: Hawezi kutoka bila kupaka make up / Mwana FA / AY / Tunagombana kila siku Salama Jabir: Hawezi kutoka bila kupaka make up...
41:42 | 112,708
IRENE UWOYA; TESSY KANICHUKULIA BWANA/NIMEFULIA/INGAWA MIMI MTAMU/DIAMOND/MZEE WA BWAX/WAMESEMA IRENE UWOYA; TESSY KANICHUKULIA BWANA/NIMEFULIA...
40:01 | 322,789
Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 2 Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 2
15:59 | 79,058


coinpayu