Okebiz Video SearchTitle:Salama Na OMMY DIMPOZ SE6 EP31 | ELEGANT PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
Duration:28:24
Viewed:0
Published:22-08-2022
Source:Youtube

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Kama kukiwa kuna mkutano wa Chama cha Watanashati hapa Africa na pengine Duniani basi Ommy Dimpoz anaweza kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Chama hiko na pengine anaweza kuwa hata Mwenyekiti. Hakuna swali juu ya utanashati wake kuanzia vivazi hadi nywele na hata kuongea. Anakumbuka utanashati wake ulianza toka alipokua mdogo sana, na wakati anakua si kama kila kitu alichokua anakitaka alikua anakipata ila alihakikisha vile vile vichache alivyokua navyo alihakikisha vinakua visaaafi na vinamkaa kweli kweli. Na tabia hiyo ya kujipenda na kuvaa vizuri ndo inamtambulisha Ommy Dimpoz kuwa ni mmoja wa wasanii wanaovaa vizuri zaidi hapa barani Afrika. Omary amekua analelewa na Bibi yake baada ya Mama yake kufariki akiwa mdogo. Anakumbuka mapenzi ambayo amekua akimuonyesha toka zamani, ni kweli kama mtoto lazima utakua unamkumbuka Mama yako, ila Bibi yake alihakikisha anapata vile vyote ambavyo mtoto anakua anahitaji. Mimi na Omary ni mtu na Rafiki yake kwahiyo mazungumzo haya zaidi yalikua ni kwaajili yako, uweze kumuelewa na kuifahamu milima na mabonde ambayo ameyapitia mpaka leo hii unamuona kasimama imara. Kama mtoto siku zote unakua unataka kumjua Baba yako na haikua tofauti kwa Ommy pia. Shuleni watoto huitwa na wazazi wao, ukiwaona wenzako wanawaleta Baba zao na wewe hujawahi kumuona au pengine ni kwa nadra sana lazima likutie unyonge. Anakumbuka Mama yake alivyofariki na jinsi ambavyo Mzee wake alikata mawasiliano ki lazima kabisa, anakumbuka kwamba Mzee wake tayari alikua na familia nyengine lakini kama mtoto anaamini na yeye pia alikua na haki ya kupata mapenzi hata kidogo tu kutoka kwake. Miaka ya hivi karibuni Mzee wake ameonekana kuutaka ukaribu nae kwa kasi kubwa sana ila kwa Omary huo umekua kama mtihani hivi, ana kinyongo nae bado na anaamini kwamba Mzee wake anataka kuwa karibu na yeye kwasababu tu ameona mwanae amekua maarufu na pengine anaonekana mambo yake mazuri. Hapo ndo panapo mtatiza yeye maana anaamini huo si upendo wa dhati, na hiyo ni sababu ya yeye kuendelea na maisha yake bila ya Baba yake. Pengine kuna siku itafika wawili hawa wataacha tofauti zao zipite na pengine watafahamiana vizuri na kuyafanya mahusiano kama Baba na mwana yastawi. Pia tunafahamu kwamba miaka miwili na nusu au mitatu iliyopita Ommy aliumwa sana, na baadhi ya watu walithubutu kusema pengine hata kuimba inaweza isiwezekane tena ila kwa Rehma za Mwenyezi Mungu alimponya na kazi yake ya muziki anaendelea kuifanya kama kawaida. Nimekua nikispend nae muda mwingi kipindi ambacho tumekua tukifanya Bongo Star Search msimu wa kumi na mbili mimi na yeye, na kwasababu tumekua tukifahamiana kwa muda nimemuona kabisa hayuko 100% ila mimi na yeye tunamshkuru Mungu kwa hali alonayo sasa maana mitihani aliyopitia ni mingi sana. Haya maisha ambayo anaishi sasa ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na hatuna budi kumshukuru yeye kwa kumpa watu kwenye maisha yake ambao walihakikisha anapata matibabu yote ya hali ya juu ili maisha yake yaweze kurudi kama zamani. Huku hilo hatukulizungumzia sana maana limeshaongelewa sana, ila tume ongea suala la ukuaji wake na mahusioano yake na familia. Urafiki wake na TID na jinsi walivyokutana. Urafiki wake na Ally Kiba, maisha yake ya shuleni na jinsi alivyokua. Urafiki wake na Diamond Platnumz na nini kilitokea kati yao. Muziki wa kizazi kipya na faida ambazo watu wana pata sasa na mahusiano yake na Chriatine ‘Seven’ Mosha na nini ambacho kimemfanya yeye afanye nae kazi. Pia tumezungumzia kutofahamiana kwake na meneja wa Diamond Platnumz Bwana Sallam Sharaff na Ommy emetuambia pia wawili hao maneno hasa yalianza kutoka wapi. Yangu matumaini uta enjoy maongezi haya na utaokota mawili matatu pia ambayo yatakusaidia kwenye maisha yako ili mambo yazidi kuwa mswano. Tafadhali Enjoy. Love, Salama. Support us through anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬ ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬ GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1H... Follow: Twitter: twitter.com/YahStoneTown Instagram: Instagram.com/YahStoneTown Facebook: facebook.com/YahStoneTown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

SHARE TO YOUR FRIENDS


Download Server 1


DOWNLOAD MP4

Download Server 2


DOWNLOAD MP4

Alternative Download :SPONSORED
Loading...
RELATED VIDEOS
Salama Na OMMY DIMPOZ SE6 EP31 | ELEGANT PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 Salama Na OMMY DIMPOZ SE6 EP31 | ELEGANT PART 2...
20:18 | 38,283
Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1 Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1
41:27 | 437,565
Salama Na JUX SE6 EP33 | IN CASE YOU DON’T KNOW PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 Salama Na JUX SE6 EP33 | IN CASE YOU DON’T KN...
24:17 | 77,643
Salama Na JK Ep 48| MSOGA UNO PART 1 Salama Na JK Ep 48| MSOGA UNO PART 1
28:27 | 518,394
Salama Na ZAHIR ZORRO SE6 EP52 | KIMULIMULI PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 Salama Na ZAHIR ZORRO SE6 EP52 | KIMULIMULI PAR...
23:57 | 6,607
Salama Na AUNTY SE6 EP32 | BASI BWANA… PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 Salama Na AUNTY SE6 EP32 | BASI BWANA… PART 1...
24:55 | 115,142
Salama Na HAJI Ep 52 | ALIYE KUTWIKA NDIYE ATAKAYE KUTUA PART 1 Salama Na HAJI Ep 52 | ALIYE KUTWIKA NDIYE ATAK...
43:34 | 121,839
Salama Na DR KUMBUKA SE6 EP41 | YAANI… PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 Salama Na DR KUMBUKA SE6 EP41 | YAANI… PART 1...
26:13 | 69,155

shopee ads

coinpayu